Tuesday, March 1, 2016

Jinsi Ya Kujua Tofauti Kati Ya Weaving Original Na Fake.

TIPS

Jinsi Ya Kujua Tofauti Kati Ya Weaving Original Na Fake.


Hapa mambo ya No Fake Zone , wadada tunaongezea sana extensions na you only look great kama umeunganishaia kitu oroginal, kuna hata zile ambazo sio original lakini zinakaa vizuri. Tatizo linakuja kwenye kuzitunza na kuzistyle mitindo unayotaka, si mnajua kuwa weave original unaweza liosha, ukalinyoosha, ukaziweka curls au hata ukazipaka rangi na bado zitakuwa nzuri na unaweza kukaa nazo kwa muda mrefu, wewe kazi yako inakuwa kuziosha tu na kubadili style lakini zile fake huwezi fanya hivo.
 Wale tunaotumia kitu chenyewe, zile original virgin human hair (Brazilian & Peruvian) , kuna mara nyingine unakuta zimechakachuliwa, zinakuwa sijui zimechanganywa na synthetic hair, basi leo nakuletea some tips zitakazokewezesha kujua kama weaving unalolitaka ni original au fake.
1.RESEARCH
Jinsi Ya Kujua Tofauti Kati Ya Weaving Original Na Fake 6
Kwanza kabisa fanya research, kama kawaida fanya research, google hiyo nywele unayoitaka, angalia original inakuja na rangi gani, maranyingi zinakuwa nyeusi tu kwani utaweza kuzipaka rangi kama unataka. Angalia zinatakiwa kuwa na urefu gani, uzito na hata wingi.
2.FANYA SMOKE TEST
Jinsi Ya Kujua Tofauti Kati Ya Weaving Original Na Fake 3
Unaweza pia ukajua kama weaving unalolitaka ni original au fake kwa kufanya smoke test, yaani chukua nywele hiyo na kuiwasha moto. Sio yote  chukua kaportion kadogo tu, sasa sijui hapo unaponunua kama utaruhusiwa kuchoma nywele kabla hujainunua  ,lakini kama ukiichoma mota na ikawa majivu kabisa basi kitu original hiko! lakini ukiichoma na ikawa kama inaganda kisha ikipoa inaganda basi ni feki!
3.WEKA MAJI
Jinsi Ya Kujua Tofauti Kati Ya Weaving Original Na Fake 5
Kama umeshanunua weaving lako na unatakakujua kama ni original weka maji, lioshe kisha jaribu kuchana. Kama nywele zimejifungafunga sana na ni tabu kuzichana basi ni feki! lakini kamaunaweza kuzichana vizuri basi kitu original.
4.RANGI
Brazilian Bundle Deals
Rangi pia ni njia nyingine ya kujua kama weaving ni original au ni fake, kama nilivyosema mwanzo maveaving original huwa yapo in natural colors, yaani rangi kama ya nywele za kawaida za mtu kabisa. Hivyo unaweza kuamua mwenyewe kama utazipaka rangi, utaziseti au utazirelax

No comments:

Post a Comment